Harmonize, Kajala, Paula wahojiwa polisi

0
383

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesema kuwa linaendelea kuchunguza tuhuma za kusambaa kwa picha za utupu za mwanamuziki Rajabu Kahali, maarufu Harmonize.

Taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Lazaro Mambosasa imeeleza kuwa tayari wamewahoji Frida (Kajala) Masanja (36) Paula Peter (18) na Raymond Mwakyusa (27) maarufu Rayvanny.

Wengine waliohojiwa kuhusiana na sakata hilo ni Claiton Revocatus maarufu Baba Levo (34), Catherine Charles na Juma Haji (32).

Mambosasa ameeleza kuwa watuhumiwa wote wapo nje kwa dhamana.