Director Khalifani afariki dunia

0
948

Mwandaaji na mwongozaji wa video za muziki nchini maarufu kama Director Khalfani Khalmandro amefariki dunia leo Mei 5, 2024 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu.

Taarifa za hivi karibuni za kuugua kwake zilizosambaa mitandaoni zilieleza kuwa Director Khalfani amelazwa hospitalini akiwa na tatizo la damu kuvilia kwenye ubongo, lililosababisha kupooza upande wa kulia wa mwili mwake.