Cillian Murphy mwigizaji bora Oscars

0
341

Mwigizaji wa Ireland, Cillian Murphy ameshinda tuzo ya mwigizaji bora kupitia filamu ya Oppenheimer kwenye tuzo za 96 za Oscar zilizotolewa usiku wa kuamkia leo huko Los Angeles, California nchini Marekani.

Oppenheimer ni filamu ya kusisimua ya mwaka 2023 iliyoandikwa, kuongozwa na kutayarishwa na Christopher Nolan ambapo Cillian Murphy ameigiza kama J. Robert Oppenheimer, mwanasayansi wa silaha za atomiki wa Marekani aliyekuwa akifanyakazi katika mradi wa Manhattan wakati wa vita ya pili ya dunia.

Murphy amewashinda wakali wengine akiwemo Paul Giamatti wa The Holdovers, Jeffrey Wright wa American Fiction na Bradley Cooper wa Maestro.

Hii ni mara ya kwanza kwa Murphy kushinda tuzo za Oscar ingawa ana historia ya kushinda mfululizo wa tuzo za awali za filamu akiwa mwigizaji bora katika Baftas na Screen Actors Guild, na mwigizaji bora katika filamu ya Golden Globes.

Je, Unakubaliana na ushindi wa Cillian Murphy kuwa mwigizaji bora Oscars?.