Beyoncé avunja rekodi ‘ni historia’

0
412

Mwimbaji, mwandishi wa nyimbo na dansa, Beyoncé Giselle Knowles-Carter kutoka nchini Marekani amekuwa msanii wa kwanza kutunzwa zaidi katika historia ya tuzo za Grammy.

Mpaka sasa Beyoncé ameshinda mara 32 katika tuzo hizo.

Tuzo iliyomweka Beyoncé juu zaidi ilikuwa albamu bora ya densi/elektroniki ambayo ameshinda kutoka kwenye albamu yake ya ‘Renaissance’.

Tuzo za Grammy kwa mwaka 2023 zimefanyika Jumapili Februari 5, 2023 nchini Marekani ambapo Beyoncé alijizolea ushindi wa tuzo nyingine mbili
Best R&B Song (Cuff It)
Best Traditional R&B Performance (Plastic Off The Sofa)

#Grammy2023