Kenny Rogers afariki dunia

0
1524

Wapenzi wa muziki wa country kutoka maeneo mbalimbali duniani , wanaendelea kuomboleza kifo cha nyota wa muziki huo Kenny Rogers aliyefariki dunia akiwa na umri wa miaka 81.

Rogers ambaye amekua katika muziki kwa muda wa takribani miaka sitini, amefariki dunia nyumbani kwake akiwa amezungukwa na familia yake.

Katika miaka ya 1970 na 1980, mwanamuziki huyo nyota wa nchini Marekani alitikisa chati mbalimbali za muziki wa country duniani na pia alifanikiwa kupata tuzo tatu za Grammy.

Katika uhai wake nyota huyo wa muziki wa Counry ambaye ni mzaliwa wa Texas, aliwika katika nyimbo mbalimbali ambazo ni pamoja na The Gambler, Lady, Islands In The Stream, Lucille, She Believes In Me, na Through the Years.

Pia alikuwa Country Music Hall of Fame member, mshindi mara sita wa tuzo za CMA , alitunukiwa CMA Willie Nelson Lifetime Achievement tuzo ya mwaka 2013, tuzo ya Mwanamuziki wa CMT of a Lifetime mwaka 2015 na alipigiwa kura kuwa ya Favorite Singer of All Time na wasomaji wa magazeti ya USA Today na People.