Buriani Gardner

0
387

Mwili wa mtangazaji wa Clouds FM Gardner Habash umeagwa leo Aprili 23, 2024 kijijini kwao Kikelelwa Kata ya Tarakea wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro ambapo pia unatarajiwa kupumzishwa kijijini hapo. Watu mbalimbali wakiwemo wafanyakazi wenzake, ndugu, jamaa na marafiki wameshiriki katika shughuli hiyo. Gardner alifariki dunia Aprili 20, 2024 katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete iliyopo mkoani Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.