Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO) imebadili mfumo wa ufugaji katika ranchi ya Taifa ya West Kilimanjaro kwa kuifanya kuwa ranchi pekee ya ufugaji wa Kondoo.
NARCO imefikia uamuzi huo lengo likiwa ni kukidhi mahitaji ya soko la kondoo la Afrika Mashariki na Kati.
Bodi ya wakurugenzi ya NARCO ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mhandisi Cyprian Luhemeja imefikia uamuzi huo baada ya kutembelea ranchi hiyo na kujionea makundi makubwa ya kondoo, huku kukiwa na uhitaji wa mifugo hiyo katika viwanda vya nyama katika nchi jirani.
Bodi ya NARCO ipo katika ziara ya kutembelea Ranchi za Taifa zinazomilikiwa na kampuni hiyo, ili kuongeza tija na mabadiliko katika sekta ya mifugo pamoja na kukidhi soko la ajira na la mifugo.