Waziri Mkuu aunda tume kushughulikia kero za Wafanyabiashara Kariakoo

0
526

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameunda tume ya watu 14 ambao watashughulikia kero za Wafanyabiasha katika Soko la Kariakoo, Dar es Salaam.

Katika timu hiyo Wajumbe saba wanatoka Serikalini na saba ni Wafanyabiashara, ambapo timu hiyo itapitia kero zote zinazowakabili Wafanyabiashara na kupata ufumbuzi.

“Kwa upande wa Serikali Ofisi ya Waziri Mkuu inamleta Katibu Mkuu wangu, wizara ya Fedha kwa kuwa Katibu Mkuu yeye ni Mlipaji Mkuu muda mwingi anakuwa ofisini, Naibu Katibu Mkuu wake anakuwa kwenye Kamati hii, wizara ya Viwanda na Biashara Katibu Mkuu wake anaingia kwenye Kamati hii….”- Amesema Waziri Mkuu.

Waziri Mkuu amesema wanaunda timu ambayo ikitoka itakuwa na majibu.

Kwa upande wa Wafanyabiashara Fred Vunjabei nae amejumuishwa kwenye Kamati hiyo ambayo itatembea maeneo yote makuu ya biashara nchini kupata changamoto na kutolewa ufumbuzi.