Moja kati ya mikakati ya serikali ya awamu ya tano ni kufikia uchumi wa kati utakaochochewa zaidi na ukuaji wa viwanda nchini
Tanzania imekuwa ikiagiza magari kutoka nje ya nchi kwa mahitaji ya ndani na hata nchi jirani kama vile Zambia, Malawi na Rwanda
Waziri wa viwanda na biashara Innocent Bashungwa ametoa maelekezo kwa wawekezaji wa kampuni ya kuunganisha magari ya GF ambao wameonesha nia yakuwekeza nchini Tanzania katika kuunganisha na kuuza magari kufanya hivyo ifikapo Mei mwaka huu
Akizungumza na TBC Mkurugenzi wa kampuni ya kuunganisha magari Imran Karmali anasema wanauwezo wakuunganisha magari 3500 kwa mwaka na kuongeza ajira kwa watanzania pindi watakapozindua kiwanda hicho