Waziri aagiza waliouziwa umeme bei ghali kurudishiwa fedha zao

0
1053

Maafisa wawili wa Kampuni ya Jumeme wamekamatwa na jeshi la polisi kwa tuhuma ya kuwauzia wananchi wa Kisiwa cha Maisome wilayani Sengerema uniti moja ya umeme kwa shilingi 3,500 badala ya TZS 100.

Wawili hao wamekamatwa kufuatia agizo lililotolewa na Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kilemani ambapo ametoa agizo hilo baada ya wakazi wa eneo hilo mkoani Mwanza kuwasilisha malalamiko kuhusu kampuni hiyo inayosambaza umeme wa jua kwa kuwauzia nishati hiyo kwa gharama kubwa.

Aidha, Waziri Kalemani amepiga marufuku kampuni za kusambaza umeme wa aina yoyote nchini kutouza uniti moja ya umeme kwa zaidi ya shilingi 100.

Katika hatua nyingine ameagiza kuandaliwa kwa orodha yenye majina ya watu wote waliotozwa gharama ya zaidi ya shilingi 100, ili uandaliwe utaratibu wa kurejeshewa fedha zao.