Washindi wa picha bora za utalii watangazwa

0
3664

Picha 20 za viumbehai wakiwemo ndege, nyuki, nyoka na nyani ni miongoni mwa picha za wapiga picha 20 walioibuka kidedea katika mashindano ya mpigapicha bora wa viumbehai vya utalii kwa mwaka 2022, katika mashindano ya ‘Wlidlife Photographer of the Year’ yaliyofanyika huko London nchini Uingereza.

Makumbusho ya historia asilia ya huko London yametangaza washindi hao huku mpiga picha kutoka nchini Marekani, Karine Aigner akinyakua tuzo ya jumla kwa kuwa na picha nzuri ya nyuki aina ya cactus wakiwa wamejivingisha kama mpira wakigombea jike.

Mpiga picha Brent Stirton naye ni miongoni mwa wapigapicha hao bora wa picha za utalii kwa mwaka 2022.

Yeye alishuhudia nyani aitwaye Ndakasi akiokolewa akiwa na umri wa miezi miwili na miaka 13 baadaye alimpiga picha tena nyani huyo aliyefia mikononi mwa mwangalizi wake, Andre Bauma katika hifadhi ya Virunga iliyopo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Ndege aina ya wren mwenye rangi ya kahawia na kijivu anayekula mizoga, mimea na wadudu alipigwa piga na Nick Kanakis wakati akitafuta chakula
katika hifadhi ya Taifa ya Tatam nchini Colombia,na hivyo kuifanya picha hiyo kuwa miongoni mwa picha bora za utalii kwa mwaka 2022.

Picha nyingine ya kuvutia ni ile ya pango la nyoka wanaoning’inia, huko Quintana Roo, Mexico ambapo mpiga picha wake ni Fernando Constantino Martnez Belmar.

Fernando alisubiri gizani huku nyoka aina ya ‘Yucatn rat’ akichomoza kichwa chake kutoka kwenye pango, ambapo maelfu ya popo walipokuwa wakitoka nje, nyoka huyo aliruka kutoka alipojificha na kuwakamata na kuwala.

Picha nyingine ambayo ni picha bora ya utalii kwa mwaka 2022 ni ile inayomuonesha ndege aina ya Houbara wa visiwa vya Canary aliponaswa akicheza na kututumua manyoya ya kifua chake kuonesha uzuri wake.

Houbara mara nyingi hupendelea kuinua manyoya kwenye sehemu ya mbele ya shingo yake, kurudisha kichwa chake nyuma, kukimbia mbele, kuzunguka nyuma na kutua kwa muda kabla ya kuanza tena kufanya hivyo.

Washindi hao wa picha 20 bora za utalii za viumbehai kwa mwaka 2022, wamechaguliwa kutoka kwenye mchuano uliojumuisha wapiga picha elfu 38 kutoka sehemu mbalimbali duniani.