Zaidi ya shilingi billioni 2.75 zimetumika kuwawezesha kiuchumi wanawake,vijana na watu wenye ulemavu 8,191 katika wilaya Nyamagana mkoani Mwanza katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.
Akizungumza katika kongamano la wajasirimali,Mkuu wa wilaya Nyamagana Dkt. Philis Nyimbi amesema kuwa fedha hizo ambazo zimewezesha wanufaika kujikwamua kiuchumi zimetolewa kupitia vikundi 848 vya wanawake,vijana na watu wenye ulemavu.
Baadhi ya wajasiriamali walionufaika na uwezeshaji wa wananchi kiuchumi wilayani nyamagana mkoani mwanza wamekutana kutathmini mafanikio yaliyofikiwa katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.
Wajasiriamali 8,191 kutoka vikundi 848 vya wanawake,vijana na watu wenye ulemavu wamenufaika na mikopo ya billioni 2.75 katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.