Wanawake na vijana kuwezeshwa katika biashara

Kongamano la Wanawake na Vijana

0
2530

Rais Samia Suluhu Hassan amesema Tanzania ni sehemu salama kwa wafanyabiashara na wawekezaji wanawake pamoja na vijana.

Rais Samia ameyasema hayo mkoani Dar es Salaam wakati akifungua rasmi mkutano wa wanawake na vijana katika biashara.

Amesema, mkutano huo utasaidia kuwawezesha wanawake na vijana kushiriki kikamilifu katika biashara ndani na nje ya nchi.

Lengo la mkutano huo ni kuwakutanisha pamoja wanawake na vijana kujadiliana, kubadilishana uzoefu na kutatua changamoto wanazokabiliana nazo katika biashara.

Kauli mbiu ya mkutano huo wa siku mbili ni wanawake na vijana: Injini ya Biashara chini ya Mkataba wa Eneo Huru la Biashara la Afrika.

Takribani washiriki 500 wanahudhuria mkutano huo ambao ni pamoja na viongozi mbalimbali Wanawake katika ngazi ya Urais, Marais wastaafu, Makamu wa Rais, Mawaziri Wakuu, Wakuu wa Taasisi za kimataifa, watu mashuhuri, Mawaziri wanaosimamia sekta za biashara na masuala ya jinsia na Wanawake, Vijana na Wafanyabiashara watarajiwa.

Mkutano huo utafungwa tarehe 14 mwezi huu na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Mwinyi.