Jeshi la polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa kushirikiana na timu maalum ya kuzuia na kupambana na uhalifu wa mitandaoni, linawashikilia watu 25 kwa tuhuma za kufanya uhalifu kwa njia ya mtandao.
Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Muliro Jumanne amesema kwa nyakati tofauti watuhumiwa hao wamekuwa wakituma ujumbe wa kidanganyifu kwa watu kwa lengo la kutapeli.
Amesema watuhumiwa hao wamekutwa wakiwa na vifaa mbalimbali ambavyo wanavitumia katika kufanya uhalifu huo.
Kamanda Muliro amesema watuhumiwa wote wamehojiwa kwa kina na taratibu za kisheria zinakamilishwa ili wafikishwe mahakamani.