Shija Kamanija ‘Vunja Bei’ ametoa zawadi ya vyombo kwa wafanyakazi wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi (MUHAS)
Huu umekuwa ni mwendelezo wa zoezi lake la kugawa vyombo katika taasisi za Serikali kati yao ni pamoja na watumishi na wafanyakazi wa MUHAS.
Vunja Bei amesema anaona fahari kutoa zawadi kwa watumishi na wafanyakazi mbalimbali kwa kuwa wanajituma sana kutimiza wajibu wao, na kuunga juhudi za Rais, Dkt. John Magufuli katika kuwatumikia Watanzania.
“Watumishi na wafanyakazi wa sekta ya afya wanajitahidi kwa kiwango kikubwa kuokoa maisha ya Watanzania na ndiyo maana napendezwa na utendaji kazi wao hadi umenifanya kuwaletea zawadi,” Vunja Bei ameeleza.
Vunja Bei amekuwa akigawa zawadi ya vyombo katika taasisi za serikali hasa katika sekta ya elimu, afya na jeshi la polisi katika maeneo mbalimbali hapa nchini.