Viwanda 4,777 vyaanzishwa nchini

0
468

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mita (TAMISEMI) Selemani  Jafo amesema kuwa jumla ya viwanda 4,777 vimenzishwa nchini kufuatia agizo la serikali la kutaka kila mkoa kuanzisha viwanda Mia Moja.

Waziri Jafo ametoa kauli hiyo jijini Dodoma wakati akizungumza na Wakuu wa Mikoa yote nchini kuhusu tathmini ya utekelezaji wa agizo la serikali la ujenzi wa viwanda Mia Moja kwa kila mkoa.

Ameongeza kuwa viwanda hivyo vimeajiri zaidi ya wafanyakazi ambao ni Watanzania Elfu Thelathini na Sita hadi sasa.

Kwa mujibu wa Waziri Jafo, viwanda hivyo 4,777 vilivyoanzishwa,  vitakuza soko la wazalishaji wa malighafi na kuzalisha bidhaa ambazo nchi ilikuwa ikiziagiza kutoka nje ya nchi.

Akizungumza wakati wa mkutano huo, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji  Ludovick Nduhiye amezitaka halmashauri nchini kutenga maeneo zaidi kwa ajili ya ujenzi wa viwanda.