Vanessa Mdee aendelea kukipaisha Kiswahili

0
1277

Msanii na Mrembo kutoka nchini Tanzania, Vanessa Mdee na mchumba wake Rotimi ambaye pia ni msanii kutoka nchini Marekani mwenye asili ya Nigeria, kwa pamoja wameandika kitabu kiitwacho ‘SWAHILI 101 vol.1’ kwa lengo la kuwasaidia watu kujua lugha ya Kiswahili na kuizungumza kwa haraka.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Vanessa na Rotimi wamezindua kitabu hicho ikiwa ni sehemu ya kukuza lugha ya kiswahili na kujifunza kwa wale ambao ni wageni wa lugha hiyo.

Mara kwa mara Vanessa amekuwa akiweka picha za video zikimuonesha akimfundisha Rotimi lugha ya Kiswahili.

Kitabu cha ‘SWAHILI 101 vol.1’ kimechapishwa na kampuni ya Independently published mwanzoni mwa mwezi huu na kina kurasa 37, huku kikiwa kinapatikana katika mtandao wa Amazon.

https://www.instagram.com/tv/CPWC4BZJazO/?utm_source=ig_web_copy_link

Kitabu hicho kinatajwa kuwa ni rahisi kubeba na kusafiri nacho kwa mtu yeyote.

‘Mtu yeyote anayeanza kujifunza Kiswahili popote duniani ni rahisi kusoma kitabu hiki,” amesema Vanessa Mdee.

“Ni kitabu ambacho kina baadhi ya maneno na misemo anayopenda Rotimi kama asante, nakupenda, Mama yangu nk, pia tumejifunza njia nzuri na ya haraka ya kujifunza lugha na kuitumia kila siku,” ameongeza Vanessa Mdee.