Uamuzi.wa ATCL kuanza safari Geita wapongezwa

0
278

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Dkt Leornad Chamuriho amesema uzinduzi wa safari za ndege za Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) kutoka Dar es salaan Kwenda Geita utasaidia kukuza shughuli za utalii nchini.

Dkt Chamuriho ameyasema hayo wakati wa hafla ya uzinduzi wa safari za ndege kutoka Dar es salaam kwenda Geita, na kuwashauri Wananchi wa mkoa huo kutumia fursa hiyo kwa kujenga hoteli za kitalii na hata kusafirisha bidhaa kutoka mkoani humo kwenda maeneo mengine.

Baadhi ya abiria waliosafiri na ndege hiyo kutoka jijini Dar es salaam kwenda Geita wameeleza kufurahishwa na kutumia muda wa takribani saa mbili tofauti na ilivyokuwa hapo awali ambapo walikuwa wakitumia.muda mrefu zaidi.

Wameipongeza Serikàli kwa kuwajali wakazi wa mkoa wa Geita na kuwafikishia karibu usafiri wa ndege wa uhakika.

Naye Mbunge wa jimbo la Chato Dkt Medard Kalemani, amewahimiza wakazi wa mkoa wa Geita kutumia fursa ya kuanza kwa safari hizo za ndege kufanya biashara na hivyo kukuza vipato vyao.