TRA yakusanya trilioni 18

0
761

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imefanikiwa kukusanya jumla ya shilingi trilioni 18.14 kwa mwaka wa fedha 2020/21 ikiwa ni wastani wa shilingi trilioni 1.51 kwa mwezi.

Katika robo ya mwisho ya mwaka huo wa fedha TRA imekusanya jumla ya shilingi trilioni 4.45 ambapo ni sawa na shilingi trilioni 1.34 Aprili, trilioni 1.35 Mei na shilingi trilioni 1.85 Juni.

Kufuatia mafanikio hayo TRA imewapongeza walipakodi wote licha ya kuwepo kwa changamoto mbalimbali ikiwemo UVIKO19 iliyoathiri shughuli za uchumi na maisha ya wananchi kwa ujumla.

Mamlaka hiyo imesema imejipanga kukuza uhusiano na walipakodi na kutatua changamoto zinazowakabili kwa haraka ikiwa ni pamoja na kutoa elimu ya kodi ili kuongeza ari ya ulipaji kodi, hatua itakayowezesha utekelezaji wa miradi ya maendeleo na huduma mbalimbali.