Sayari inayofanana na Dunia yagunduliwa

0
732

Shirika la Anga za Juu la Marekani (NASA) Jumanne wiki hii limegundua Sayari nyingine yenye ukubwa sawa na Sayari ya Dunia inayoitwa TOI 700e.

TOI 700e inalingana na Dunia kwa asilimia 95 na sehemu kubwa inaundwa na mwamba katika muundo wake ambayo pia kwa mujibu wa NASA sayari hiyo ni mojawapo ya mifumo michache iliyo na sayari nyingi ndogo.

Ugunduzi huu unakuja miezi michache baada ya NASA hapo awali kugundua sayari nyingine tatu katika mfumo huo, moja wapo ikiwa katika eneo wanaloweza kuishi binadamu.