Ni mwanamke kwa mara ya kwanza

0
2395

Kwa mara ya kwanza Umoja wa Mataifa umemchagua mwanamke kuwa Katibu Mkuu wa Muungano wa Kimataifa wa Mawasiliano (ITU).

Doreen Bogdan Martin raia wa Marekani, amechaguliwa kumrithi Houlin Zhao ambaye aliitumikia nafasi hiyo tangu nwaka 2014.

Doreen Bogdan Martin amemshinda mpinzani wake kutoka Russia, Rashid Ismailov baada ya kupata kura 139 dhidi ya mpinzani wake aliyepata kura 25.

Anatarajiwa kuanza kipindi chake cha uongozi kama Katibu Mkuu wa Muungano wa Kimataifa wa Mawasiliano Januari Mosi mwaka 2023.

Mwanamke huyo atauongoza muungano huo mkongwe zaidi wa Umoja wa Mataifa ambao unawajibika na shughuli za mawasiliano ya kimataifa.

Shughuli hizo ni pamoja na kugawa mizunguko ya Setilaiti duniani kote, kuboresha miundombinu duniani na kuratibu viwango vya kiufundi.