Wananchi wakiendelea kulia na changamoto ya vifurushi vya simu kuisha haraka, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetoa ufafanuzi wa sababu kadhaa ambazo zinachangia hali hiyo kutokea.
Katika kikao baina ya mamlaka hiyo na wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya habari, Dk. Emmaniel Manase, Mkurugenzi wa Masuala ya Kisekta wa TCRA amebainisha mambo yanayoweza kusababisha tatizo hilo ambalo baadhi ya wananchi hawalifahamu.
Dk. Manase akabainisha kwamba, vifurushi vinaweza kuisha mapema kutokana na kuongezeka kwa kasi ya mitandao na simu janja (smartphone).
Anasema, unakuta simu ilikuwa na laini ya 3G, ukahamia 4G, “sasa wakati anafurahia simu ina pakua haraka inakula kwa kasi vifurushi na si kasi tu ubora wa video na picha inaongezeka, “ubora wa hayo unapoongezeka na matumizi ya bando yanaongezeka.”
Jambo jingine anasema, simu janja zinapokuja, “oparetion system [mfumo endeshi] zinaongezeka, zinakuwa kubwa na zamani ulikuwa unatumia 2GB kufanya update [maboresho], lakini tunatumia application nyingi sana na hizi zinafanyiwa update mara kwa mara na Watanzania walio wengi hatuna njia nyingine kutumia intanet nje ya simu zetu.”
Dk. Manasema anasema, watumiaji wengi wa simu, unakuta inapakua background bila wewe kujijua. Lakini uwepo wa application nyingine ambazo hazitumii na zinaongeza matumizi ya data.
Ili kukabiliana na tatizo hilo na kuwasaidia watumiaji, Dk. Manasema anasema, “tumewaelekeza watumiaji wa huduma kuandaa application kuonesha umebakiza sms, data na dakika ngapi, ili mtumiaji wa simu awe anaona kile anachokitumia.”