Selous kubaki kwenye Urithi wa Dunia

0
367

Tanzania imeshinda katika utetezi wake ilioutoa kwenye Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO),  ambapo shirika hilo lilitaka kuliondoa pori la akiba la Selous kwenye orodha ya Urithi wa Dunia.

 

UNESCO ilitaka kufanya uamuzi huo kutokana na kutekelezwa kwa ujenzi wa mradi wa bwawa la kufua umeme wa maji la Julius Nyerere (JNHPP) katika mto Rufiji.
 
Pori la akiba la Selous litabaki katika orodha ya Urithi wa Dunia, huku mradi huo wa kuzalisha Megawati 2, 115 za umeme ambao kwa sasa umefika asilimia 54 ukiendelkea na utakamilika mwezi Juni mwaka 2022.