SAMAKI MPYA

0
4039

Wanasayansi wamegundua aina mpya ya samaki wa kundi la ‘Psychedelic Fish Species’ mwenye mwonekano unaofanana na upinde mvua.

Wanasayansi katika Pwani ya Maldives wamegundua aina hiyo mpya ya samaki ambaye ana rangi angavu, ni kiumbe chenye rangi ya waridi kilichopewa jina la rose-veiled fairy wrasse au Cirrhilabrus finifenmaa’

Samaki mpya ni kiumbe mdogo mwenye kichwa cha rangi ya waridi na mwili wenye vivuli vya rangi ya bluu, kwa ujumla Samkai huyu amepatikana kati ya futi 131 na 229 chini ya usawa wa bahari, kielelezo cha rangi ya upinde wa mvua ni ugunduzi wa kushangaza na wa kwanza kuainishwa rasmi na mtafiti.