NFRA yatakiwa kuongeza kasi ununuzi wa mahindi

0
4810


Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeutaka Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) kununua tani laki moja za zao la mahindi kutoka kwa Wakulima wa maeneo mbalimbali nchini, ili kuiwezesha nchi kuwa na akiba ya kutosha ya mahindi.
 
Wito huo umetolewa jijini Dodoma na Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo, wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari.
 
Chongolo amesema hatua ya NFRA kununua mahindi kutoka kwa wakulima pia itasaidia kutatua changamoto ya kukosekana kwa soko la zao la mahindi inayowakabili wakulima wengi nchini.
 
Katibu Mkuu huyo wa CCM ametumia mkutano wake na waandishi wa habari kuishauri Serikali kutafuta namna bora ya kupunguza bei za mbolea, ambazo zimepanda kwa kasi kutokana na janga la corona.