MTN Rwanda kusitisha uuzaji wa vocha za kukwangua

0
1803

Kampuni ya Mawasiliano ya Simu ya MTN tawi la Rwanda (MTN Rwanda), imetangaza kusitisha uuzaji wa vocha za simu za kukwangua kuanzia tarehe 15 mwezi huu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kampuni hiyo, huduma ya kuongeza salio kwenye simu itapatikana kwa njia ya kielektroniki na kununua kupitia huduma za fedha kwenye simu.

Huduma hiyo ya kuongeza salio kwenye simu kwa njia ya Kielektroniki nchini Rwanda itarahisisha na kuongeza uharaka wa uongezaji wa vocha pamoja na kupunguza uchafunzi wa mazingira.