Mradi wa Bomba la EACOP ni salama

0
2442

Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Dkt. James Mataragio ambaye ni pia ni mjumbe wa bodi ya Shirika linaloendesha mradi wa ujenzi wa Bomba la kusafirisha mafuta ghafi la Afrka Mashariki (EACOP ) amesema mradi huo umefuata sheria za kimataifa katika utekelezaji wake.

Dkt. Mataragio amesema hayo katika kongamano la kujadili tija na usalama wa mradi wa bomba la mafuta kutoka Hoima , Uganda hadi Chongoleani Mkoani Tanga , lililofanyika Mkoani Dar es Salaam.

Amesema utekelezaji wa mradi huo umefuata taratibu zote za kimataifa na sheria za Tanzania kwa kuhakikisha kwamba haki za binadamu zinazingatiwa wakati wa kuwahamisha wananchi ambao maeneo yao yatapitiwa na mradi.

Ameongeza kuwa Serikali ya Tanzania na Uganda pamoja na wabia wapo tayari kwa mradi ambapo hadi sasa zipo benki zimetoa uhakika wa kutoa fedha kwaajili ya mradi huo.

Amesema mradi utagharimu dola za marekani bilioni 5.1 ambapo hadi sasa mradi huo umeshapata nusu ya fedha hizo.