Mpango wa SANVN Viwanda Scheme waanza kwa mafanikio

0
300

Serikali imeanzisha mpango wa uendelezaji wa viwanda vidogo na vya kati (SANVN Viwanda Scheme), unaolenga kuongeza mnyororo wa thamani katika uzalishaji wa bidhaa na kutatua changamoto ya upatikanaji ujuzi, masoko na mitaji.

Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) Beng’i Issa amesema mpango huo umeanzishwa ili kukuza sera ya viwanda, kuwapatia Wajasiriamali fursa ya kupata mitaji yenye masharti nafuu pamoja na kuwajengea uwezo katika kuandika maandiko ya biashara.

Ameongeza kuwa mpango huo wa SANVN Viwanda Scheme unalenga kukuza hifadhi ya jamii kupitia viwanda na kampuni ambazo zitaendelezwa.

“Mpango huu umekuwa na mafanikio makubwa ndani ya miezi 11 ya mwanzo, kwani mpaka sasa mikopo yenye thamani ya shilingi milioni 900 imekwisha tolewa kwenye Makampuni yapatayo nane katika Mikoa ya Mwanza, Arusha, Kilimanjaro na Dar es Salaam,” amesema Beng’i Issa.