Katika mahojiano maalum na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) ikiwa ni mwaka mmoja wa Serikali ya awamu ya sita madarakni, Rais Samia Suluhu Hassan ameeleza mpango wa Serikali yake katika kuboresha bandari.
KUTAFUTA WABIA
“ Bandari inafanya vizuri kwa makusanyo lakini tukichukua hatua itafanya vizuri zaidi, tunachukua hatua kwanza tunatafuta wabia wa kuendesha bandari na unapokuwa na mbia hatakubali ya kienyeji yaendelee pale, mbia tutakwenda naye kwenye kurekebisha mifumo.”
TUTAREKEBISHA MIFUMO YA BANDARI
“Kurekebisha mifumo na kuweka mifumo madhubuti itakayosomeka bandari na itakayosomeka na taasisi ya kukusanya mapato TRA na itakayosomana na maeneo yote ambayo matumizi na ukusanaji wa mapato unahusika”
KUREKEBISHA PORT MANAGEMENT ( UONGOZI WA BANDARI)
“Pia tunakwenda kurekebisha port management (uongozi wa bandarini), tumechukua hatua za kubadilisha uongozi lakini bado tunakwenda kuunda bodi mpya bandarini, tumeshapata wenyeviti wapya kusimamia vizuri”
KUREKEBISHA JINSI YA UNUNUZI WA MAFUTA
“Bandari kuna masuala ya mafuta, ushushaji wa mafuta na upakiaji huko nako kuna upotevu, tunakwenda kusimamia na kurekebisha jinsi ya ununuzi wa mafuta, kurekebisha kuweka kodi, kuweka kumbukumbu za mafuta lakini hata stoke ya mafuta “