Mkonge wa Tanga wawavutia Wajerumani

0
339

Na Bertha Mwambela Tanga

Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Regina Hejs amefika mkoani Tanga kujionea fursa za uwekezaji kwenye zao la mkonge.

Zao la Mkonge ni moja kati ya mazao saba ya kimkakati yaliopo hapa nchini.

Siku za hivi karibuni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alitoa agizo kwa halmashauri ambazo mikoa yao inalima mkonge kutenga hekari 10 kwa ajili ya kuotesha mbegu za zao hilo na kuzigawa kwa wananchi wanaolima kwenye maeneo yao.

Mpaka sasa serikali imekiwezesha Kituo cha Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) Mlingano kilichopo wilayani Muheza mkoani Tanga kuandaa mbegu bora za mkonge zitakazosambazwa kwenye maeneo mengine hapa nchini.

Aidha, serikali inakusudia kuongeza uzalishaji wa zao la mkonge kutoka tani 37,000 za sasa mpaka kufikia tani 120,000 ifikapo mwaka 2025.