Mjadala wa mabadiliko ya uchumi duniani

0
668

Mweka Hazina kutoka benki ya CRDB Olais Tira amesema, uchumi wa Taifa unaweza kuathirika zaidi kutegemea namna ambavyo Taifa husika limejipanga kukabiliana na athari zitokanazo na mdororo wa kiuchumi duniani.

Akizungumza mkoani Dar es Salaam katika mjadala wa mabadiliko ya uchumi duniani, athari na suluhisho kwa Mwananchi wa kawaida Tira amesema, nchi nyingi za Afrika zilikuwa na ukuaji mzuri wa uchumi japo kwa sasa zimeonekana kuathiriwa na mdororo wa kiuchumi ikiwemo Tanzania.

Akitoa suluhisho la mdororo huo amesema Taifa linapaswa kuwa na mbinu za kuamua namna gani litajikita kujiandaa kukabiliana na athari zitokanazo na mdororo wa kiuchumi ili kupunguza athari zitokanazo na mdororo huo.

Akitolea mfano janga la UVIKO -19, Mweka Hazina huyo wa benki ya CRDB amesema, Tanzania iliweza kukabiliana na changamoto hiyo kwa mbinu ilizotumia kipindi hicho, hali iliyochangia kuwa na athari ndogo ikilinganishwa na nchi nyingine.