Madalali wapigwa stop kupewa vibanda Samunge

0
1537

Serikali Mkoani Arusha imetoa utaratibu wa kugawa upya Vibanda vya biashara katika soko la Samunge lililoungua kwa moto mwishoni mwa mwezi machi na kuonya madalali kutopewa vibanda kwa ajili ya kupangishia Wafanyabiashara wadogo.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha , Mrisho Gambo ametoa utaratibu huo wakati wa zoezi la kugawa vibanda katika soko hilo lililopo katikati ya jiji la Arusha baada ya kuwepo utata kwa baadhi ya Watu waliokuwa wanamiliki vibanda zaidi ya kimoja na kuvipangisha kwa gharama kubwa