Machinga kupata soko Kigoma

0
1933

Rais Samia suluhu Hassan ameuagiza uongozi wa mkoa wa Kigoma kuhakikisha wafanyabiashara wadogo maarufu kama Machinga wanakuwa na mazingira bora ya kufanyia shughuli zao.

Rais Samia ametoa agizo hilo alipokuwa akizungumza na wakazi wa mkoa wa Kigoma katika uwanja wa Lake Tanganyika, wakati akihitimisha ziara yake ya siku nne mkoani humo.

Amewaambia wakazi wa mkoa wa Kigoma kuwa, ziara yake mkoani humo ilikuwa na lengo la kuunyanyua mkoa huo na kuufanya kuwa kitovu cha biashara kwa mikoa ya magharibi.

Rais Samia amewashukuru wananchi wa mkoa wa Kigoma kwa kujitokeza kwa wingi kila alipokuwa akipita kuwasalimia na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo.

‘ULAKOZE CHANE KIGOMA’ ndio neno lake la mwisho kwa wakazi wa Kigoma likiwa na maana asante sana Kigoma.