Kiswahili kitumike kufanya biashara

0
1969

Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji amezihamasisha nchi za Afrika kutumia lugha ya kiswahili, ili kuondoa changamoto ya lugha katika kufanya biashara.

Aidha Waziri Kijaji amewataka wafanyabiashara wa Tanzania kuzalisha bidhaa zenye viwango vya kimataifa, ili kikidhi usindani wanapotumia fursa za soko la Eneo Huru la Biashara Afrika ( AfCFTA)

Waziri Kijaji ameyasema hayo nchini Niger wakati akishiriki mkutano wa ngazi ya Baraza la Utendaji la Mawaziri, katika mkutano wa 17 wa dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika kuhusu Maendeleo ya Viwanda Barani Afrika unaoendelea mjini Niamey.

Waziri Kijaji atamwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan katika mkutano huo ngazi ya wakuu wa nchi na Serikali unaotarajiwa kufanyika hapo kesho.