Kampuni ya Barrick Gold yailipa Tanzania bilioni 231 za malimbikizo ya kodi

0
1053

Kampuni ya madini, Barrick Gold Corporation imeanza kuilipa serikali ya Tanzania malimbikizo ya kodi ambayo inadaiwa kutokana na shughuli zake za uchumbaji madini nchini.

Leo Waziri wa Fedha na Mipango wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango amepokea hundi kifani ya dola milioni 100 (shilingi 231 bilioni) kutoka kwa mwakilishi Mkazi wa Kampuni ya Barrick, Hilaire Diarra.

Fedha hizo ni sehemu ya malipo ya dola milioni 300 (shilingi 694 bilioni) ambazo kampuni hiyo ilikubali kuilipa serikali Tanzania kumaliza mzozo uliokuwepo kati ya Serikali na Kampuni hiyo.

Mzozo huo ulipelekea kuanzishwa kwa kampuni ya ubia ya madini ya Twiga kati ya serikali na Kampuni ya Barrick.

Hafla hiyi imehudhuriwa pia na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ambaye pia alikuwa Mwenyekiti wa Timu ya Serikali ya Majadiliano na Barrick, Prof. Palamagamba Kabudi, Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo na Meneja wa Mgodi wa North Mara, Luiz Correia