Hoteli hii ipo nchi mbili tofauti

0
1405

Hoteli hii ndogo inayoendeshwa na familia ‘Hotel Arbez Franco-Suisse’, pia inajulikana kama L’Arbézie.

Upekee wa hoteli hii ni mahali ilipo ambapo ipo katika mpaka wa kimataifa.

Uwepo wa hoteli Arbez Franco-Suisse katika eneo hilo ni matokeo yasiyotarajiwa ya mkataba wa mwaka 1862 wa Dappes, ambapo Ufaransa na Uswisi zilikubaliana kubadilishana eneo dogo ili kuruhusu udhibiti kamili wa Ufaransa wa barabara ya kimkakati iliyo karibu.

Kifungu katika mkataba huo kilieleza kuwa majengo yote yaliiyopo katika eneo la mpaka yatabaki mahali pake, hali iliyomwezesha mjasiriamali kufungua duka na baa katika eneo hilo mwaka 1921.

Matokeo yake ni kwamba nusu ya hoteli hiyo iko Ufaransa na nusu nyingine iko nchini Uswisi, huku mpaka wa kimataifa ukigawanya mgahawa na vyumba kadhaa.