Hifadhi ya Taifa ya Serengeti yaibuka kidedea Afrika

0
349

Kamishna Msaidizi Mwanadamizi wa Uhifadhi – Mawasiliano, Pascal Shelutete amesema Hifadhi ya Taifa ya Serengeti imeibuka na ushindi huo baada taasisi ya World Travel Awards (WTA) ya nchini Marekani kuzishindanisha hifadhi mbalimbali kwa njia ya mtandao.

Hifadhi hizo ni pamoja na Center Of Calahari (Botswana), Etosha (Namibia), Kidepo Valley (Uganda), Kruger (Afrika Ya Kusini) na Maasai Mara Nationa Reserve (Kenya).

Aidha, Shirika la Hifadhi Tanzania (TANAPA) linaishukuru serikali, wadau wa utalii pamoja na wananchi waloipigia kura hifadhi ya Serengeti na kuibuka mshindi kwa mara ya pili , ambapo mwaka 2019 ilishinda tuzo hizo.