Elon Musk: Sizitaki mbichi hizi

0
1314

Tajiri wa dunia, bilionea Elon Musk ameghairi kuendelea na mchakato wa kuununua mtandao wa Twitter kwa dola bilioni 44 za kimarekani.

Musk ambaye ni mmiliki wa magari ya umeme ya Tesla na kampuni ya SpaceX inayotengeneza vifaa vya kuruka angani, ameishutumu kampuni hiyo ya Twitter kwa kuwa na uwakilishi wa uongo na wa kupotosha wa akaunti zilizofunguliwa.

Barua ya mawakili wa Twitter kwenda kwa mawakili wa Musk imebainisha kuwa Twitter haijakiuka makubaliano yoyote ambayo tayari yalikwishafikiwa wakati wa mchakato huo, na kwamba tatizo lipo kwa tajiri huyo.