Kufuatia agizo la Waziri Mkuu Kassim Majaliwa la kuzitaka Taasisi za fedha chini ya Benki Kuu ya Tanzania, kuanzisha kitengo maalum ndani ya taasisi hizo kitakachokuwa kinapokea madini ya dhahabu kama dhamana ya mkopo kwa wachimbaji wa madini ikiwa ni sambamba na kuangalia namna ya kupunguza riba ili iwe nafuu kwa wachimbaji wadogo, bank ya NBC imeanza kutekeleza agizo hilo na kutambulisha aina hiyo ya dhamana kwa ajili ya kutoa mikopo
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa Biashara Elvis Ndunguru, amesema NBC imefanya tathmini ya kina na kuhakikisha kuwa watanzania wanaendelea kunufaika na huduma zao na kutengeneza mfumo rafiki kupata mikopo kwa wawekezaji na wachimbaji wadogo kutumia madini ya dhahabu kama dhamana yakupata mkopo
Benki ya NBC ambao kwa sasa ndio wadhamini wakuu wa ligi kuu soka Tanzania Bara wameendelea kuwa wadau wakubwa katika sekta wa madini nchini na kuanza kwa dhamana hiyo ya mkopo kutawanufaisha na kutoa kipaumbele kwa wachimbaji wadogo wa madini