Chapati ‘Rolex’ yenye 204kg yavunja rekodi Uganda

0
4469

Chapati ‘Rolex’ kubwa zaidi yenye kilo 204.6 (451 Ib) imepikwa na Raymond Kahuma na wenzake nchini Uganda na kuifanya ivunje rekodi ya ukubwa nchini humo.

Raymond na wenzake wamefanya kazi ya maandalizi kwa miezi kadhaa ili kuandaa chapati hiyo kwa ajili ya kuweka rekodi na kuhakikisha kila kitu kinakwenda sawa.

Chapati ya ‘Rolex’ ya Uganda imepimwa na ina urefu wa mita 2.32 na unene wa mita 0.66 kwa (thickest diameter).

Chapati ‘Rolex’ ni chakula cha mtaani maarufu nchini Uganda, kina changanyika na mayai ‘omelette’ na mboga inayofunikiwa na kuzungushiwa kwenye chapati.

Ni moja ya chakula pendwa mtaani kwa sababu kinatayarishwa kwa uharaka na kinaweza kuliwa wakati wowote kutoka kifungua kinywa, chakula cha mchana au chakula cha jioni au kutumika kama kitafunwa.

Jina “Rolex” linatokana na njia yake ya utayarishaji, uviringishaji wa pamoja wa chapati na mayai ‘omelette rolled’ au mazagazaga mengine.

Wazo hilo lilitokana na ubunifu wa wauza chapati katika mkoa wa Busoga “Wabasoga” kisha wazo likaenea hadi Wandegeya karibu na Chuo Kikuu cha Makerere nchini Uganda, likichochewa na wanafunzi waliohitaji mlo wa haraka kwa sababu ya ufinyu wa muda na bajeti.