Benki Kuu ya Tanzania (BOT) imechukua usimamizi wa China Commercial Bank Limited na kusimamisha Bodi ya Wakurugenzi na uongozi wa benki hiyo ya nchini China baada ya kubaini upungufu mkubwa wa mtaji kinyume na matakwa ya sheria ya mabenki na taasisi za fedha nchini.
Uamuzi huo umetangazwa jijini Dodoma na Gavana wa Benki Kuu Profesa Florens Luoga katika mkutano wake na waandishi wa habari.
Profesa Luoga amesema shughuli za utoaji wa huduma kwa wateja wa China Commercial Bank Limited zinasimama kuanzia leo kwa kipindi cha siku Tisini ili kuipa nafasi BOT kutathmini hatua za kuchukua na kupata ufumbuzi.