Watu 19 wafariki kwa kunywa pombe yenye sumu

0
374

Watu 19 wamefariki dunia nchini Morocco na wengine wamelazwa hospitalini baada ya kunywa pombe kwenye kibanda kilichopo pembeni mwa barabara.

Mamlaka nchini humo zimeeleza kwamba mtuhumiwa mwenye umri wa miaka 48 anashikiliwa na polisi kwa kuhusika na tukio hilo.

Ukaguzi wa polisi umebaini lita 50 za kileo hicho kinachoaminika kuwa ndio chanzo cha vifo katika kibanda cha mtuhumiwa.

Kati ya watu 30 waliofikishwa hospitalini wakiwa na hali mbaya, wawili bado wapo chini ya uangalizi maalumu.

Taarifa kutoka nchini humo zinaeleza kwamba waathirika hao walipata maumivu ya kichwa, kutapika na maumivu ya tumbo.

Tukio kama hilo lilitokea mwezi Julai mwaka 2021 ambapo watu zaidi ya 20 walifariki dunia huko Oujda, mashariki mwa Morocco.