Waliopandikizwa Uloto warejea nyumbani

0
196

Hospitali ya Taifa Muhimbili imeendelea kuweka historia kwa kutoa huduma ya matibabu ya kibobezi ya upandikizaji wa Uloto (Bone Marrow Transpalnt) kwa wagonjwa watano wenye Saratani ya damu, na hivyo kufikisha wagonjwa 16 waliopatiwa matibabu hayo toka huduma hiyo ianzishwe hospitalini hapo.

Wagonjwa hao waliokaa hospitalini hapo kwa muda wa siku 14 , leo wameruhusiwa kurejea nyumbani baada ya matibabu yao kukamilika na afya zao kuendelea kuimarika.

Akizungumza na wasndishi wa habari mkoani Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Profesa Mohamed Janabi amesema wagonjwa waliopo kliniki kwa sasa ambao wanahitaji kupandikizwa Uloto ni zaidi ya 150 kwa mwaka.

Amesema wagonjwa wanaotakiwa kupandikizwa Uloto ni wale wenye changamoto ya kansa za damu, kushindwa kwa uloto kuzalisha chembechembe za damu pamoja na wenye ugonjwa wa Selimundu (Sickle Cell).