Bilioni moja wana unene hatarishi duniani – utafiti

0
231

Zaidi ya watu bilioni moja wanaishi na unene unaosababisha uzito uliokithiri duniani kote. Hii inahusisha takribani watu wazima milioni 880 na watoto milioni 159, utafiti wa karibuni wa kimataifa unaonesha.

Kwa mujibu wa utafiti huo, nchi zenye watu wanene zaidi duniani ni Tonga na Samoa kwa wanawake; na Samoa na Nauru kwa wanaume. Katika nchi hizo zenye idadi ndogo ya watu, asilimia 70 hadi 80 ya watu wazima wana uzito kupita kiasi.

Kati ya nchi 190 zilizofanyiwa utafiti, kwa nchi za Afrika Misiri ndio yenye idadi kubwa ya wanene, wengi wakiwa wanawake.

Utafiti uliofanywa mwaka jana ulionesha kwamba zaidi ya nusu ya watu duniani watakuwa na unene kupita kiasi ifikapo 2035 endapo hatua za kudhibiti tatizo la unene hazitachukuliwa.

Unene unaweza kuongeza hatari ya mtu kupata magonjwa yasiyoambukiza kama ugonjwa wa moyo, kisukari na aina kadhaa za saratani.

Wewe msomaji unajiepushaje na unene?