Basi la UDART lateketea kwa moto

0
246

Basi la Kampuni ya Usafiri wa Mabasi yaendayo Haraka jijini Dar es salaam (UDART) limeshika moto na kuteketea katika eneo la Kimara mwisho jijini Dar es Salaam usiku huu.

Watu walioshuhudia tukio hilo wamesema kuwa, basi hilo lilikua likitokea maeneo ya katikati ya jiji kuelekea Kimara Stendi.

Chanzo cha moto huo bado hakijafahamika na hadi sasa hakuna taarifa za majeruhi au vifo kutokana na tukio hilo.