Ronaldo ajivunia kuwa bora kwenye soka

0
589

Nyota wa Juventus, – Cristiano Ronaldo amesema anajivunia kuwa miongoni mwa wachezaji wachache waliowika kwa muda mrefu kwenye soka la kiushindani.

Akizungumza wakati wa usiku wa tuzo za UEFA, – Ronaldo amesema kuwa, kwa kiasi kikubwa amekuwa bora kwenye soka kwa sababu ya ushindani uliopo kati yake na Lionel Messi, ushindani anaoamini umechangia pia kwa Messi kuendelea kuwika.


Amesema kitendo cha yeye na Messi kutawala kwa zaidi ya miaka kumi kwenye tuzo za wachezaji Barani Ulaya na Duniani, ni ushahidi kuwa yeye na Messi ni wachezaji wa pekee kuwahi kutokea.

Ronaldo ameongeza kuwa anaamini ataendelea kutamba kwa miaka kadhaa ijayo kwani bado anajiona yupo timamu kimwili.