Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amewataka wakazi wa mkoa wa Kigoma hususani wanaoishi katika maeneo ya mipakani na mwambao wa ziwa Tanganyika kuchukua tahadhari za kiusalama dhidi ya ugonjwa wa Ebola.
Akizungumza kwenye mikutano ya hadhara katika kata za Mwakizega na Kazuramimba wilayani Uvinza mkoani Kigoma, Makamu wa Rais pamoja na mambo mengine amewataka wakazi hao kuacha tabia ya kupokea na kuwahifadhi wageni kutoka nchi jirani.
Kuhusu lishe Makamu wa Rais amewataka watendaji wa sekta ya afya pamoja na wazazi hususani akina mama kutimiza wajibu wao.
Aidha Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amewataka wavuvi na wafanyabiashara wa mazao ya uvuvi katika ziwa Tanganyika kujiunga kwenye vikundi ili kuunganisha nguvu katika uendelezaji wa shughuli zao.
Katika wilaya ya UVINZA Makamu wa Rasi pia amekagua mradi wa ukarabati wa kituo cha afya cha Uvinza.
Katibu Mkuu Wizara ya Uvuvi Dkt. Rashid Tamatama ametumia fursa ya ziara ya Makamu wa Rais mkoani Simiyu, kutangaza kuanza kwa oparesheni ya kuwasaka wavuvi haramu katika ziwa Tanganyika.