Baada ya kufanyika kwa tathmini ya Ligi Kuu Tanzania msimu uliopita, Bodi ya ligi imeamua kupunguza timu zitakazoshiriki katika ligi hiyo kutoka 20 na kufikia 16 kama ilivyokuwa hapo awali.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi,- Boniface Wambura amewaambia Waandishi wa habari jijini Dar es salaam kuwa, baada ya kukutana na makocha na viongozi wa vilabu na kufanya majadiliano, wameamua kufanya marekebisho katika uendeshaji wa ligi hiyo ikiwa ni pamoja na kupunguza idadi ya timu.
Katika Ligi daraja la kwanza, timu Nane zitashuka moja kwa moja kwenda ligi daraja la Pili, lakini kutakuwa na michezo ya mtoano ili kupata timu za kubaki Ligi Kuu na za kushuka daraja.
Katika hatua
nyingine Wambura amesema kuwa, katika msimu huu mpya wa Ligi, timu mwenyeji wa
mchezo inatakiwa kuwa na gari la kubeba wagonjwa, lakini pia viwanja ambavyo
havijafanyiwa marekebisho vinatakiwa kufanyiwa kabla ya ligi kuanza.