Bodi ya Maziwa yavunjwa

0
203

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina, ameivunja Bodi ya Wakurugenzi ya Bodi ya Maziwa nchini kuanzia hii leo.

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini cha wizara hiyo imesema kuwa, Waziri Mpina amefanya uamuzi huo kutokana na mamlaka aliyonayo kisheria, chini ya Sheria ya Bodi ya Maziwa Namba 8 ya mwaka 2004 kifungu cha 8 na 9 (1).

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Waziri Mpina amefikia uamuzi wa kuivunja Bodi hiyo ya Wakurugenzi ya Bodi ya Maziwa nchini, kutokana na kutoridhishwa na utendaji wake.