Mashambulio yaongezeka Burkina Faso

0
199

Askari Kumi wa Jeshi la Burkina Faso wameuawa katika shambulio lililofanywa na Wanamgambo kwenye  jimbo la Soum, lililopo eneo la Kaskazini la nchi hiyo.

Habari kutoka Burkina Faso zinasema kuwa,  askari wengine wengi wamejeruhiwa katika tukio hilo lililotokea katika  jimbo hilo la Soum ambalo lipo kwenye mpaka wa nchi hiyo na Mali.

Kufuatia shambulio hilo, Jeshi la Burkina Faso limeanzisha operesheni ya kusawaka Wanamgambo hao ambapo pia limejiandaa kwa mashambulio ya anga na yale ya ardhini.

Kumekua na mashambulio ya kushtukiza kwenye majimbo kadhaa ya nchi hiyo katika siku za hivi karibuni, mashambulio yanayodaiwa kufanywa na Wanamgambo wa Kiislamu hasa katika eneo la Kaskazini na Mashariki mwa nchi hiyo.

Mamia ya watu wameuawa katika mashambuli hayo nchini Burkina Faso katika kipindi cha kuanzia mwaka huu hadi hivi sasa, huku watu wengine Laki Moja na Nusu wakiyakimbia makazi yao.

Mwezi Disemba mwaka 2018, hali ya tahadhari ilitangazwa  katika majimbo mbalimbali ya nchi hiyo,  na vikosi zaidi vilisambazwa katika majimbo hayo kwa lengo la kukabiliana na washambuliaji.